Juventus Wazindua Rasmi Jezi Mpya Ya 2026-27

Juventus wamezindua rasmi jezi yao ya nyumbani kwa msimu wa 2026-27, ikiwa ni muonekano mpya wa kisasa unaoendelea kubeba utambulisho wao wa jadi wa mstari mweusi na mweupe. Klabu hiyo ya Serie A imeeleza jezi hiyo kama tafsiri ya kisasa ya mistari maarufu ya wima inayowatambulisha duniani kote.

Juventus Wazindua Rasmi Jezi Mpya Ya 2026-27

Jezi hiyo mpya imebeba muundo wa kipekee wenye kola ya polo, ikirudisha kumbukumbu za jezi za kihistoria zilizovaliwa na magwiji wa klabu hiyo. Kwa kuongeza ladha ya kisasa, rangi ya dhahabu imeongezwa kwenye nembo ya klabu, alama ya adidas na namba za wachezaji, ikionyesha hadhi na hadithi ya Juventus ndani ya soka la Ulaya.

Katika taarifa yao rasmi, Juventus wameeleza falsafa ya jezi hiyo kwa maneno mizizi ya kina, tukielekea mbele. Wamesema muundo mpya unachanganya historia na ubunifu wa kisasa, huku ukitoa muonekano wa kujiamini na nguvu inayohitajika kwenye mashindano ya leo.

Juventus Wazindua Rasmi Jezi Mpya Ya 2026-27

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Jezi hiyo pia inakamilishwa na bukta nyeupe zenye michoro ya dhahabu na mistari meusi, pamoja na soksi nyeupe. Ni mchanganyiko wa urithi na ubunifu unaoifanya Juventus kubaki na utambulisho wake wa kipekee.

Juventus Wazindua Rasmi Jezi Mpya Ya 2026-27

Mbali na muonekano, jezi hiyo imetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ya adidas CLIMACOOL+, inayosaidia wachezaji kubaki na ubaridi kupitia uingizaji hewa ulioboreshwa. Kwa sasa, jezi hiyo tayari inapatikana madukani na mtandaoni, huku mashabiki wakianza kuupokea muonekano mpya wa Bianconeri kwa hamu mkubwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.