Timu ya Juventus imefanikiwa kubeba kombe la Coppa Italia kwa mara ya 14 sasa baada ya ushinda wa 2-1 dhidi ya Atalanta hapo jana.
Katika mechi iliyoonekana kuwa na usawa huku timu zote zikishambulia kwa wakati tofauti tofauti, Mabingwa wa Kihistoria wa Serie A walikuwa washindi kwa magoli ya Kulusevski na Chiesa, huku Morata akionekana kupoteza magoli ya wazi mara kadhaa katika mchezo huo.
Ushindi huo wa jana umewafanya Vijana wa Turin kuchukua kombe hilo kwa mara ya 14 sasa na kuweka rekodi ya kuwa timu iliyochukua kombe hilo kwa mara nyingi zaidi, ikifuatiwa na As Roma waliobeba mara tisa.
Katika mchezo huo wachezaji wa Juventus, Cuadrado, Chiesa na Kulusevski waling’aa kwa kuonesha mchezo mzuri sana kwa nafasi zao. Kombe hilo lilifurahiwa sana na wachezaji wa Juventus kutokana na ukweli kuwa msimu huu umekuwa msimu mgumu kwa wana hawa wa Turin.
Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.
Magdalena
Pongezi kwao
Sauda
Safi sana