Klabu ya Juventus inatajwa kufikiria kuwasilisha ofa ya mkopo kwa mshambuliaji wa Chelsea, Nicolas Jackson, katika dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi, huku ikilenga kuongeza nguvu katika safu yake ya ushambuliaji.
Ripoti zinaeleza kuwa Jackson kwa sasa yupo kwa mkopo katika klabu ya Bayern Munich, lakini mabingwa hao wa Bundesliga hawajaridhishwa na kiwango chake na hivyo hawana mpango wa kumbakisha msimu ujao. Hali hiyo imefungua milango kwa klabu nyingine kuanza kumfuatilia kwa karibu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Juventus inaonekana kuwa na uhitaji mkubwa wa mshambuliaji mpya kutokana na kushuka kwa kiwango cha safu yao ya ushambuliaji msimu huu katika mashindano ya ndani na ya kimataifa. Uongozi wa klabu hiyo unaripotiwa kuona Jackson kama chaguo la muda mrefu na lenye uwezo wa kuboresha kikosi.
“Klabu kadhaa zinamfuatilia Jackson kutokana na hali yake ya sasa ya mkataba na nafasi yake ndani ya Chelsea,” imeelezwa na vyanzo vya karibu na mchezaji huyo.
Kwa upande wake, Jackson ameripotiwa kuwa ameieleza timu yake ya uwakilishi kwamba hana mpango wa kurejea tena ndani ya Chelsea, na kwamba anapendelea ama kuuzwa au kupelekwa kwa mkopo wa msimu mmoja ili kupata muda zaidi wa kucheza mara kwa mara.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal mwenye umri wa miaka 24 amecheza mechi 33 katika mashindano yote msimu huu akiwa na Bayern Munich, akifunga mabao 10. Mkataba wake na Chelsea unatajwa kuendelea hadi mwaka 2033, huku uamuzi kuhusu hatma yake ukitarajiwa kufanyika katika dirisha lijalo la usajili.


