OFISA Habari wa Yanga Ali Kamwe amesisitiza kuwa kipigo hakikwepeki kwa klabu ya Al Hilal kutoka kwa klabu yao na hawatafungwa mabao chini ya matatu kwa kuwa wanataka kuimalizia mechi hiyo wakiwa hapa kwa Mkapa.

Kamwe alisema wanajua kuwa ubora wa Al Hilal upo kwenye historian a midomo ya watu na wao wanakwenda kuonyesha kuwa Yanga ya sasa ni bora zaidi ya Al Hilal kwa kuwafunga kwenye mech izote mbili ambazo watacheza.

Akiweka bayana juu ya mipango yao kuelekea kwenye mchezo huo ambao unatarajiwa kesho kutwa Jumamosi kwenye uwanja wa Mkapa Kamwe alisema kila kitu kimekuwa tayari kwa upande wao na kilichosalia ni kwenda kuzimaliza dakika 90 uwanjani.

“Wale Al Hilal tunakwenda kuwafunga mabao siyo chini ya matatu hapa kwetu, halafu kule kwao tutajua jinsi gani tunakwenda kumalizia mchezo huo. Mpango wetu ni kuumaliza mchezo huu hapa nyumbani.

“Narudia tena kusema, ubora wa Al Hilal umebaki kwenye historia tu ya mambo ambayo waliyafanya zamani kwenye mashindano haya. Lakini kiuhalisia ni kwamba hawana timu bora kama zamani.

“Hivyo sisi Yanga, tunataka kwenda kuionyesha dunia kuwa tuna timu bora kuliko timu nyingine yoyote kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati,” alisema Kamwe.

Yanga watashuka dimbani Jumamosi hii kucheza mchezo wa kwanza wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kisha mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Oktoba 15 nchini Sudan.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa