Karia Atoa Neno kwa U23

RAIS wa Shirikisho la Soka nchini, Wallace Karia amewataka wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 23 kuacha unyonge na kuipambania nafasi ya kufuzu AFCON.

Timu hiyo inaendelea na maandizi ya mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Sudan kwenye Uwanja wa JMK Park ambapo wanatarajia kucheza Septemba 23, mwaka huu.

Akizungumza baada ya mazoezi hayo leo, Karia amesema kuwa: “Nawaomba tuache unyonge na tuende kupambana hasa kwa ajili ya taifa letu.

“Tutakuwa na wenzetu wanajeshi ambao watakuwa wanawafundisha uzalendo na kupambana kitu ambacho tunafundisha kwa timu zote za taifa.

“Tuna imani mnaenda kupambana kwa ajili ya kuhakikisha mnapata nafasi ya kufuzu AFCON.”

Acha ujumbe