Kipa El-Shanawy Afungiwa Mechi Nne Baada Ya Kumshambulia Mwamuzi

Kipa wa klabu ya Al Ahly na timu ya taifa ya Misri, Mohamed El-Shenawy, amefungiwa mechi nne kufuatia tukio la kumshambulia mwamuzi kwa kumpiga kichwani baada ya mchezo dhidi ya Ceramica Cleopatra kumalizika kwa sare ya 1-1.

Kipa El-Shanawy Afungiwa Mechi Nne Baada Ya Kumshambulia MwamuziAdhabu hiyo ilitangazwa Alhamisi na Ligi Kuu ya Misri, ikieleza kuwa kipa huyo pia ametozwa faini ya pauni 50,000 za Misri (takriban dola 942) kwa kosa la kumshambulia mwamuzi kwa kutumia mkono, ingawa bila vurugu kubwa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Tukio hilo lilitokea baada ya Mohamed El-Shenawy kukasirishwa na uamuzi wa mwamuzi kukataa ombi la penalti kwa Al Ahly katika dakika za nyongeza, kufuatia madai ya mpira kugonga mkono wa mchezaji wa upinzani.

Kipa El-Shanawy Afungiwa Mechi Nne Baada Ya Kumshambulia MwamuziKwa mujibu wa taarifa ya ligi, “Amefungiwa mechi nne na kutozwa faini ya pauni 50,000 za Misri kwa kosa la kumshambulia mwamuzi kwa kumsukuma au kumvuta kwa mkono (matumizi ya mkono bila vurugu).”

Adhabu hiyo inamaanisha kuwa Mohamed El-Shenawy atakosekana uwanjani hadi wiki ya mwisho ya hatua ya mtoano ya ligi, hali ambayo ni pigo kwa Al Ahly katika mbio za ubingwa.

Kipa El-Shanawy Afungiwa Mechi Nne Baada Ya Kumshambulia MwamuziKwa sasa, Al Ahly wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 41, wakiachwa kwa pointi tano na vinara Zamalek.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.