Tuisila Kisinda ambaye alikuwa ni mchezaji wa zamani wa Yanga amerejea klabuni hapo kwa mara nyingine akitoka Morroco ambapo alikuwa akiichezea timu ya RS Berkane nchini humo. Kisinda alitambulishwa jana kabla dirisha la usajili kufungwa na timu ya wananchi.
Mchezaji huyo ambaye anacheza kwenye nafasi ya winga mshambuliaji alisajiliwa na Yanga msimu juzi akitokea klabu ya AS Vita ya nchini Congo ambapo alidumu kwa wananchi ambapo alicheza msimu mmoja tuuh na baadae kutimkia Berkane.
Baada ya kuondoka kwenye Morroco alikutana na mchezaji mwingine ambaye ni Cloutus Chama aliyekuwa akicheza Simba. Kwahiyo Tuisila Kisinda na Chama wakakutana Berkane ambapo walikuwa wakicheza timu moja lakini Cloutus Chama kabla ya msimu kuisha alirejea kwenye klabu yake ambayo ni Simba na sasa amerejea tena.
Kwa vyanzo mbalimbali vya habari Kisinda akiwa na Berkane amecheza michezo 36 huku akiwa amefunga bao moja, na akitoa pasi za mwisho nne tu. Mashabiki na wapenzi wa mpira wanasubiri kile ambacho ataenda kukitoa kwenye klabu ya Yanga ambao ndio mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC.