Kiungo wa Dortmund Reinier Aambukizwa Corona.

Kiungo wa Borussia Dortmund Reinier amepimwa na kukutwa maambukizi ya virusi vya corona, klabu hiyo ya Ujerumani imethibitisha.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18, ambaye alijiunga na Dortmund kwa dili ya mkopo wa miaka miwili akitokea Real Madrid mwezi Agosti amefanyiwa vipimo vya COVID-19 bada ya kutoka kwenye majukumu na timu ya taifa ya Brazil ya vijana wenye umri chini ya miaka 21 wiki iliopita.

Reinier hakuwa sehemu ya kikosi cha Dorrtmund ambacho kilicheza na Hertha Berlin na kupata ushindi wa 5-2 wikendi iliyopita na hakuna mchezaji mwingine wa BVB ambaye amekutwa na maambukizi.

Dortmund imethibitisha habari hizo siku ya Jumatatu siku moja kabla ya mchezo wa Champions League na Club Brugge, na iliongeza kwamba kinda huyo alionesha dalili na kwa sasa amejitenga.

Ametumiwa mara saba na Lucien Favre na michezo yote alitokea benchi.

Reinier, ambaye ameshinda taji Campeonate Brasileiro na Copa Libertadores akiwa na Flamengo mwaka 2019bado hajafunga, kutoa asisti wala kutengeneza katika michezo mitatu ya Bundesliga na amefanikiwa kupiga shuti moja tu.


Usichelewe Kukamata Mkwanja Huu!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

 

20 Komentara

    duh pole sana kwake inambidi afate masharti ili aweze kupona haraka

    Jibu

    Duuuuh pole yake

    Jibu

    Pole sana Reinier.

    Jibu

    Jamani pole sana

    Jibu

    Get well soon

    Jibu

    Pole Sana kijana.

    Jibu

    Duu pole yake

    Jibu

    Pole Sana

    Jibu

    Pole sana

    Jibu

    Pol san

    Jibu

    Corona ni tishio sana muda huu

    Jibu

    Dhuu pole sana

    Jibu

    Ugua pole

    Jibu

    Dah hii corona sasa ni shida

    Jibu

    Pole sana

    Jibu

    Pole sanaaa

    Jibu

    Pole

    Jibu

    Pole

    Jibu

    Pole sana

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

Acha ujumbe