Kikosi cha Timu ya KMC FC kimerejea Jijini Dar es Salaam jana na leo kimeanza mazoezi kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa siku ya Ijuma OKtoba 07 katika uwanja wa Uhuru hapa Jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni inayodhaminiwa na Meridian Bet chini ya kocha Mkuu , Thierry Hitimana ilirejea jana mapema alfajiri na hivyo kupumzika kabla ya leo kuanza maandalizi ya mchezo mwingine dhidi ya Ruvu Shooti ambapo KMC FC itakuwa nyumbani.

KMC Wanazitaka Tatu za Namungo

KMC FC inajiandaa na mchezo huo ambao ni wapili kuchezwa ikiwa nyumbani kati ya michezo mitano ambayo imeshacheza hadi sasa na kwamba jitihada kubwa na mikakati ni kuhakikisha kuwa licha ya Ligi kuwa naushindani mkubwa lakini kama Timu inajiandaa kuwapa burudani  itakayoambatana na matokeo mazuri kwenye mchezo huo.

Aidha kwa upande wa Afya za wachezaji wamerejea wakiwa na hari, morali nzuri isipokuwa Ibrahimu Ame pamoja na Hance Masoud ambao waliumia kwenye mchezo  dhidi ya Namungo uliopigwa siku ya Jumamosi ya Oktoba moja katika uwanja wa Majaliwa Ruangwa Mkoani Lindi.

“ Tumerejea jana alfajiri kutoka Ruangwa, ambapo tulikuwa kwenye mchezo dhidi ya Namungo, tumerudi salama, na tulipumzika na leo tumeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo unaokuja dhidi ya Ruvu, tunafahamu ushindani wa mchezo huo namna ulivyo, lakini tutafanya maandalizi yetu vizuri kwakuwa malengo ni kupata alama tatu.

“Kwenye ligi hivi sasa unapo kwenda kukutana na mpinzani wako, kila mmoja anakuwa amejipanga vizuri, na hii nikutokana na ushindani uliopo, hivyo na sisi kama Timu ya KMC tunajiandaa vema, mchezo upondani ya uwezo wetu na siku zote Timu bora haiwezi kukosa alama tatu muhimu mara mbili, tumekosa dhidi ya Namungo na sasa tunajipanga dhidi ya Ruvu Shooting,” alisema Christina Mwagala msemaji wa timu hiyo.

KMC FC hadi sasa ipo kwenye nafasi ya tisa ikiwa imecheza michezo mitano na kujikusanyia jumla ya alama sita na magoli sita ambapo michezo ambayo tayari imeshacheza ni dhidi ya Coast Union ya mkoani Tanga, Polisi Tanzania ya mkoani Kilimanjaro, Simba ya Jijini Dar es Salaam, Ihefu ya Mbarali mkoani Mbeya pamoja na Namungo ya Ruangwa mkoani Lindi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa