WAKITARAJIA kucheza kesho dhidi ya Ihefu, Uongozi wa KMC umeitangazia vita Ihefu na kutangaza kuwa wanahitaji pointi tatu kwenye mchezo huo.

Mchezo huo ambao awali ulikuwa upigwe Septemba 17 uliahirishwa na sasa utapigwa kesho jumanne kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

KMC, KMC Waitangazia Vita Ihefu, Meridianbet

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema: “Kikosi chetu kipo salama na tunamuomba Mungu awaamshe salama wachezaji wetu ili waende kupambana.

“Tangu kuanza kwa msimu huu hatujawahi kupata pointi tatu hivyo kwa maandalizi tuliyofanya tunahitaji hizo pointi tatu.

“Tunajua wenzetu hali yao sio nzuri na wao wanahitaji pointi tatu lakini kwa upande wetu tunazihitaji zaidi kwani hatujazipata tangu kuanza kwa msimu huu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa