Arteta Atoa Taarifa ya Majeruhi Kabla ya Mchezo Dhidi ya Southampton

Kocha mkuu wa Arsenal FC, Mikel Arteta amesema huenda wachezaji Martin Odegaard na Jurrien Timber wakarejea uwanjani katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Southampton FC.

Arteta Atoa Taarifa ya Majeruhi Kabla ya Mchezo Dhidi ya SouthamptonHata hivyo, Arteta amethibitisha kuwa mshambuliaji wa England, Noni Madueke hatakuwepo kutokana na majeraha, akijiunga na orodha ya wachezaji waliokumbwa na matatizo ya kiafya katika kikosi hicho.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza na waandishi wa habari, Arteta alisisitiza umuhimu wa uwazi kuhusu hali za wachezaji akisema “Tunapotoa taarifa kuhusu hali ya kila mchezaji, tunakuwa waaminifu kila wakati na maamuzi ya kitabibu yalifanywa kwa uwazi kabisa.”

Arteta Atoa Taarifa ya Majeruhi Kabla ya Mchezo Dhidi ya SouthamptonKocha huyo aliongeza kuwa klabu inajivunia kuwa na wachezaji wengi wanaoitwa kwenye timu za taifa, licha ya changamoto za majeraha “Inatufanya tujivunie kuwa na wachezaji wengi kwenye timu za taifa. Wachezaji wanatamani kuchezea nchi zao, na sisi tunaunga mkono hilo pale inapowezekana.”

Madueke alipata jeraha la goti wakati wa mchezo wa kirafiki wa England dhidi ya Uruguay, hali iliyomfanya kuukosa mchezo dhidi ya Japan, ingawa Arteta alibainisha kuwa jeraha lake si kubwa kama ilivyohofiwa awali.

Arteta Atoa Taarifa ya Majeruhi Kabla ya Mchezo Dhidi ya SouthamptonWakati huo huo, Arteta hakufichua idadi kamili ya wachezaji watakaokuwa tayari kwa mchezo huo, huku Bukayo Saka, Declan Rice na wengine wakitajwa kuwa kwenye uangalizi maalum, akisisitiza “Tupo katika nafasi ambayo tunahitaji kikosi imara zaidi ili kushinda kila mashindano, tukiwa tumebakiza michezo michache kufikia hatua muhimu ya FA Cup.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.