Shirikisho la Soka la Ivory Coast (FIF) limetangaza kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Emerse Fae, ameondoka rasmi kwenye wadhifa wake baada ya mkataba wake kumalizika Julai 31, 2026, huku ukiachwa bila kuongezwa. Taarifa hiyo ilitolewa Ijumaa, ikihitimisha kipindi cha mafanikio makubwa chini ya kocha huyo.
Fae alichukua mikoba ya kuinoa Ivory Coast katikati ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2024 baada ya Mfaransa Jean-Louis Gasset kutimuliwa kufuatia matokeo mabaya katika hatua ya makundi. Awali aliteuliwa kwa muda, lakini baadaye akathibitishwa kuwa kocha wa kudumu baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa taji la tatu la AFCON kwa kuifunga Nigeria mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali.
mpira wa miguu, kubeti mpira wa miguu, bashiri soka, soka, beti kwenye soka, odds za soka, bashiri mpira wa miguu, beti za soka, beti mechi za soka, odds za kubeti mpira wa miguu
Mbali na mafanikio ya AFCON, Fae aliiongoza pia Ivory Coast kufuzu michuano ya Dunia 2026, ambapo timu hiyo ilifika hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza kabla ya kuondolewa na Norway katika hatua ya 32 bora.
Katika taarifa yake, Shirikisho la Soka la Ivory Coast lilimpongeza Fae kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya timu ya taifa na kueleza kuwa mafanikio aliyoyapata yataendelea kuwa sehemu muhimu ya historia ya hivi karibuni ya soka la nchi hiyo.
“Mkataba wa Bw. Emerse Fae, kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ivory Coast, ulimalizika Julai 31, 2026 na hautaongezwa. Maendeleo na mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wake yataendelea kuwa sehemu muhimu ya historia ya hivi karibuni ya soka la Ivory Coast,” ilisema sehemu ya taarifa ya Shirikisho la Soka la Ivory Coast (FIF), ambalo pia limeeleza kuwa jina la kocha mpya litatangazwa baadaye.


