Kocha wa timu ya taifa ya Misri, Hossam Hassan, amesema bado hajafanya uamuzi wa kama mshambuliaji nyota Mohamed Salah ataanza katika mchezo wa hatua ya 32 bora ya micchuano ya Dunia dhidi ya Australia utakaochezwa Ijumaa mjini Dallas. Salah anaendelea kupona majeraha ya msuli wa nyuma wa paja aliyoyapata katika sare ya 1-1 dhidi ya Iran.
Salah alirejea kufanya mazoezi kwa sehemu Jumatano baada ya kuumia, huku akitarajiwa kuisaidia Misri iliyofuzu hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza katika historia yake ya mashindano ya Dunia. Hata hivyo, Hassan amesema hatakuwa tayari kuhatarisha afya ya nyota huyo ikiwa bado hajawa fiti kwa asilimia 100.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Salah ni mchezaji mwenye ari kubwa na anatamani kucheza, lakini sitachukua hatari yoyote mpaka nijiridhishe kuwa yuko fiti kabisa kwa ajili ya mchezo wa kesho,” amesema Hossam Hassan.
Salah tayari ameifungia Misri bao moja katika mashindano haya, akifunga katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya New Zealand kwenye hatua ya makundi. Kocha Hassan amemsifu nahodha huyo kwa kiwango chake, akieleza kuwa ameonyesha uwezo mkubwa zaidi ya matarajio ya wengi tangu aanze kufanya kazi naye.
“Australia wana wachezaji wenye nguvu na miili mikubwa, lakini hilo halitupi hofu. Soka halichezwi kwa urefu wa mchezaji, bali kwa ubora wa mchezo. Tuko tayari kukabiliana na changamoto yoyote,” amesema Hassan.


