Konate Aaga Liverpool, Enzi ya Ukuta wa Reds Yafikia Mwisho

Mashabiki wa Liverpool wamepokea taarifa nzito baada ya kuthibitishwa kuwa beki wa kati kutoka Ufaransa, Ibrahima Konate, ataondoka klabuni mwishoni mwa msimu huu baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba mpya. Mkataba wa nyota huyo unamalizika Julai 1, huku mazungumzo yaliyodumu kwa miezi kadhaa yakishindwa kuzaa matunda.

Konate Aaga Liverpool, Enzi ya Ukuta wa Reds Yafikia Mwisho

Kwa muda mrefu, Konate amekuwa akihusishwa na kuhamia Real Madrid, jambo lililozidi kuongeza presha kuhusu hatma yake Anfield. Hata hivyo, mwezi Aprili beki huyo mwenye miaka 27 aliwahi kuwapa matumaini mashabiki kwa kusema kuwa alikuwa karibu kusaini mkataba mpya na Liverpool. Kauli hiyo sasa imeonekana kupotea hewani baada ya kuthibitishwa kuwa ataondoka rasmi majira haya ya kiangazi.

Kuondoka kwa Konate kunakuja sambamba na mastaa wengine wawili wakubwa, Mohamed Salah na Andrew Robertson, ambao pia wataachana na Liverpool baada ya mikataba yao kuisha. Watatu hao walikuwa sehemu muhimu ya kikosi kilichotwaa ubingwa wa Premier League msimu wa 2024/25 na wameondoka wakiwa mashujaa wa kweli wa Anfield.

Konate Aaga Liverpool, Enzi ya Ukuta wa Reds Yafikia Mwisho

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika kipindi chake Liverpool, Konate amecheza michezo 183 kwenye mashindano yote, akitwaa mataji mbalimbali ikiwemo Premier League, FA Cup, Carabao Cup mara mbili pamoja na Community Shield. Ushirikiano wake wa kipekee na nahodha Virgil van Dijk uliifanya safu ya ulinzi ya Liverpool kuwa moja ya ngumu zaidi Ulaya chini ya makocha Jurgen Klopp na Arne Slot.

Konate Aaga Liverpool, Enzi ya Ukuta wa Reds Yafikia Mwisho

Sasa Liverpool wanakabiliwa na kazi kubwa ya kuziba pengo lake, lakini tayari wameanza maandalizi ya sajili mpya. Kijana Jeremy Jacquet mwenye miaka 20 ataungana rasmi na klabu Julai 1 akitokea Rennes, huku Giovanni Leoni naye akitarajiwa kurejea baada ya kuuguza jeraha baya la ACL.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.