Kiungo wa Atletico Madrid Geoffrey Kondogbia yupo huenda akacheza mechi dhidi ya timu yake ya zamani Valencia baada ya hali yake kuonekana kuimarika hii ni kwa mujibu wa kocha wa Atletico Diego Simeone.

Kondogbia bado hajacheza mchezo woeote kwa Atletico tangu asajiliwe mwezi Novemba 3, lakini Simeone anadhani kueleka mchezo wa Jumamosi wakiwa ugenini dhidi ya Valencia kwenye LaLiga.

Atletico wanacheza wakiwa na rekodi ya kushinda mechi tano za ligi mfululizo, na nne kati hizo alipata clean sheet hii inamaanisha wapo nyuma ya vinara wa LaLiga Real Sociedad kwa tofauti ya alama wakiwa na michezo miwili mkononi.

“Kondogbia anauwezekano mkubwa wa kucheza mechi ya Jumamosi,” Simeone ambaye amepoteza mara mbili katika michezo 21 dhidi Valencia aliongea kuhusu kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27.

“Amekuwa na maendeleo mazuri katika mazoezi na tunamuhitaji awe na kiwango kikubwa.

“Ni mchezaji imara sana, mkubwa sana na anahitaji kuwa na hali nzuri kiafya kabla hajacheza katika ubora wake.

Simeone aliulizwa kuhusu hali ya mshambuliaji wa Serbia Saponjic, ambaye bado hajauanza msimu anaweza kucheza namba tisa inategemea na hali za mastarika Luiz Suarez na Diego Costa.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa