Kostas Manolas raia wa kigiriki na beki wa zamani wa klabu ya As Roma ya nchini Italia amefanikiwa kujiunga na klabu ya Sharjah Fc ya umoja wa falme za kiarabu akitokea klabu ya Olympiacos ya nchini Ugiriki.

Beki huyo amejiunga na klabu hiyo baada ya kudumu kwa muda wa miezi sita katika klabun ya Olympiacos ya nchimi kwao baada ya kutoka katika klabu ya Napoli nchini Italia.

kostas manolasManolas ambaye amewahi kucheza katika klabu ya As Roma ya nchini Italia na anakumbukwa zaidi pale As Roma ilipopindua meza dhidi ya Barcelona katika dimba la Estadio Olympico huku goli la tatu lililoizamisha Barca akifunga beki huyo wa kigiriki.

Beki huyo pia ameitumikia klabu ya Napoli ambayo alijiunga nayo akitokea klabu ya As Roma mwaka 2019 kabla ya kuamua kurudi nyumbani ,wezi januari mwaka katika klabu ya Olympiacos na sasa ameelekea Sharjah Fc iliopo katika falme za kiarabu.JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa