Kifo cha gwiji wa soka ulimwenguni Diego Maradona kimeshitua watu wengi na kimefanya kuwa habari kubwa kwenye vyombo vya habari sehemu mablimbali dunia.

Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 60 amefariki siku ya Jumatano mjini Buenos Aires, wiki mbili tangu aruhusiwe kutoka hospitali ambako alifanyiwa upasuaji wa ubongo.

Baada ya habari kutangazwa na chama cha mpira cha Argentina habari zimeenea kila sehemu siku ya Alhamisi zimeandikwa katika kurasa za mbele na nyuma za magazeti ulimwenguni kote.

Hapa tumekukusanyia Vichwa vya habari kutoka magazeti mbalimbali siku moja baada ya Kifo cha Maradona.

Gazeti la nchini kwake Cronica limeandika “Adios” ikimaanisha “Kwaheri” likiwa na picha yake juu ya kombe la dunia.

Kurasa za Mbele za Magazeti Kuhusu Kifo cha Maradona.
Kurasa ya mbele ya gazeti la Cronica kuhusu Maradona.

Clarin wao wameweka picha ya Maradona akiwa ameshika kombe la Dunia na kicha habari kikiwa na maneno “Conmocion mundial: murio Diego Maradona” (Dunia misukosuko: Diego Maradona amefariki).

Gazeti la nchini Uruguay El Observador wameandika “A que planeta te fuiste” maana (Sayari gani uliyo kwenda?)

El Pais, gazeti la kispanish wamesema mchezaji huyo wa Barcelona alikuwa “Un dios del football” wakimaanisha Maradona alikuwa (“Mungu wa mpira wa miguu).

Pia gazeti lingine la Spain MARCA kurasa ya mbele ilikuwa “Kama ni kifa nataka nizaliwe tena nataka niwe mcheza soka….na ninataka niwe Diego Armando Maradona tena”.

Nchini Ufaransa, L’Equipe kurasa ya mbele waliweka picha ya Maradona akiwa maevalia rangi ya blue na nyeupe za bendera ya taifa lake likiwa na kichwa cha habari “Dieu est mort” wakimaanisha (Mungu amekufa).

Kicker la Ujerumani kurasa za mbele waliweka tarehe ya kuzaliwa ya Maradona na tarehe aliyo fariki chini waliweka picha yake akiwa na jezi ya Argentina.

The Mirror kichwa cha habari kilikuwa: “Diego Maradona, shujaa, mbaya, mdanganyi na Jiniazi…..amefariki akiwa na miaka 60.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

19 MAONI

  1. Kwa kweli tutamkumbuka sana tunakumbuka alipotoka kwenye matibabu yake aliahidi kuwa itakuwa sana pamoja na wanasoka wengine na hatakuwa katika makundi mabaya

  2. Kwa kweli tutamkumbuka sana tunakumbuka alipotoka kwenye matibabu yake aliahidi kuwa itakuwa sana pamoja na wanasoka wengine na hatakuwa katika makundi mabaya

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa