Nyota kijana wa Hispania, Lamine Yamal, amesema hafikirii sana kuhusu kufunga mabao bali anajikita katika kuisaidia timu yake kutwaa taji la Dunia 2026. Kauli hiyo ameitoa baada ya Hispania kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ubelgiji katika hatua ya robo fainali, huku yeye akiendelea kuwa na bao moja pekee kwenye mashindano hayo.
Yamal mwenye umri wa miaka 18 alisema mafanikio ya timu ndiyo jambo la msingi kuliko takwimu binafsi. “Bila shaka natamani kufunga mabao, lakini siingii uwanjani nikifikiria hilo. Nafikiria jinsi ya kuisaidia timu. Tukishinda Kombe la Dunia, hakuna atakayejali kama nilifunga mabao au la, muhimu ni ushindi wa timu,” alisema mshambuliaji huyo wa Barcelona.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Licha ya kutofunga mara nyingi, Yamal anaamini mchango wake unaonekana kupitia namna anavyowavuta mabeki wa wapinzani na kuwapa nafasi wenzake. “Najua ninaweza kusaidia hata nisipofunga. Harakati zangu huwafanya wapinzani wengi kunifuata na hivyo kuwapa nafasi wachezaji wengine. Kila mara nafanya kila niwezalo kwa manufaa ya timu,” alieleza.
Yamal alikumbusha kuwa hata katika Euro 2024, ambako Hispania ilitwaa ubingwa, alifunga bao moja pekee lakini hilo halikuzuia timu yake kutwaa taji. “Wapo wanaosema nilipaswa kufunga zaidi kama ilivyokuwa Euro, lakini tulitwaa ubingwa nikiwa nimefunga bao moja tu. Hata sasa nina bao moja, hivyo sina presha yoyote,” alisema huku akitabasamu.
Hispania sasa itakutana na Ufaransa katika hatua ya nusu fainali, ambapo Yamal anaamini timu yake haina sababu ya kuogopa. “Kuna uwezekano mmoja kati ya miwili; ama wao wafike fainali ya tatu mfululizo ya michuano ya Dunia au sisi tuwafunge kwa mara ya tatu mfululizo. Tutaona kitakachotokea, lakini sisi hatuwaogopi hata kidogo,” alisema nyota huyo wa Hispania.


