Wachezaji wa timu ya taifa ya Hispania, Lamine Yamal na Pedro Porro, walifanya mazoezi tofauti na wenzao siku ya Alhamisi wakati kikosi hicho kilipoanza maandalizi ya fainali ya michuano ya Dunia dhidi ya Argentina, itakayochezwa Jumapili mjini New Jersey, Marekani. Wawili hao walionekana wakifanya programu maalum ya mazoezi katika kituo cha mazoezi cha Red Bull New York.
Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF) limethibitisha kuwa Yamal na Porro wanatarajiwa kuwa fiti kwa mchezo wa fainali, huku mazoezi yao ya pekee yakielezwa kuwa ni sehemu ya mpango wa kusimamia uchovu na kulinda utimamu wa miili yao kabla ya mechi hiyo muhimu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha Luis de la Fuente alieleza baada ya ushindi dhidi ya Ufaransa katika nusu fainali kuwa Pedro Porro alikuwa akisumbuliwa na maumivu madogo. Taarifa zinaeleza kuwa beki huyo ana tatizo dogo la msuli wa nyuma ya paja (hamstring), lakini halionekani kuwa la kutisha. Kwa upande wa Lamine Yamal, hali yake inaelezwa kuwa nzuri licha ya kupata maumivu na michubuko kufuatia pambano gumu dhidi ya Lucas Digne na Theo Hernandez.
“Wote wawili wanatarajiwa kuwa tayari kwa mchezo wa Jumapili. Mazoezi yao ya tofauti ni hatua ya tahadhari katika usimamizi wa kiwango cha kazi na uchovu wa wachezaji,” lilieleza Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF), likisisitiza kuwa hakuna hofu kuhusu ushiriki wao kwenye fainali.
Hispania sasa ina siku tatu za kujiandaa na kuzoea hali ya joto na unyevunyevu wa New Jersey kabla ya kuivaa Argentina katika fainali. Wachezaji wengine wa kikosi walimaliza mazoezi yao kwa utulivu na morali ya juu, huku benchi la ufundi likilenga kuhakikisha kikosi kizima kinaingia uwanjani kikiwa katika kiwango bora cha utimamu wa mwili.


