Joan Laporta amethibitisha kurudi katika kinyang’anyiro cha kiti cha Urais katika klabu ya Barcelona.

Laporta mwenye umri wa miaka 58 aliiongoza Barcelona kutoka mwaka 2003 mpaka 2010 na kuona Barca ikipata mafanikio mengi na kuwa na ushindani mkubwa Ulaya.

Wakati w utawala wake Barca ilishinda mataji 12, ikihusisha mataji manne ya LaLiga na mawili ya Champions League akiwa na makocha kama Frank Rijkaard na Pep Guardiola.

Bartomeu na bodi ya uongozi walijiuzulu mwezi Oktoba siku chake kabla mashabiki na wanachama wa Barcelona hawajapiga kura kukosa imani na rais.

“Kuwa rais wa Barcelona ni heshima na ilinipa miaka bora zaidi katika miasha yangu na kurudi tena kuwa rais ni changamoto kubwa katika maisha yangu.” Laporta alisema siku ya Jumatatu.

“Kama wajumbe wataniamini, na shawishika kusema tutarudi katika ubora wetu, tutafanya huku tukiwa na imani na sisi wenyewe.

Ujio wa Rijkaard na Ronaldinho katika mwaka alichaguliwa Laporta uliifanya apate mafanikio makubwa kama kupata ubingwa wa ligi mfululizo mwaka 2004-05 na 2005-06 bila kusahau ubingwa wa Champions League mwaka 2006.

Laporta pia alimleta Pep Guardiola kuwa kocha mkuu wa timu ya wakaubwa ya Barcelona mwaka 2008 maamuzi ambayo yalipelekea klabu kushinda mataji makubwa matatu ndani ya msimu mmoja.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Laporta, Laporta Athibitisha Kugombea Tena Urais Barcelona., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

16 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa