Le Bris: Arsenal Ndio Timu Bora Ulaya Kwa Sasa

Kocha wa Sunderland, Régis Le Bris, amewapa heshima kubwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Arsenal, akisema kwa sasa wanaonekana kuwa timu bora zaidi barani Ulaya kutokana na kiwango wanachoonyesha ndani ya uwanja.

Le Bris: Arsenal Ndio Timu Bora Ulaya Kwa SasaKauli hiyo ya Le Bris imekuja wakati Sunderland ikijiandaa kuikabili Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa kwenye dimba la Stadium of Light. Kocha huyo amesema kikosi cha Mikel Arteta kinaonekana kuwa imara katika kila eneo, jambo linalofanya mchezo huo kuwa mtihani mkubwa kwa Sunderland.

“Ingawa bado ni mapema kwenye msimu, wanaonekana kuwa imara kila mahali, kuanzia benchi lao hadi kila idara. Kwa sasa nadhani wao ndio timu bora zaidi Ulaya,” alisema Le Bris.

Le Bris: Arsenal Ndio Timu Bora Ulaya Kwa SasaPamoja na kutoa sifa hizo, Le Bris amewataka wachezaji wake wasiingie uwanjani kwa hofu kutokana na ukubwa wa mpinzani wao. Badala yake, amesisitiza umuhimu wa Sunderland kucheza kwa kujiamini na kuendelea kushikilia utambulisho wao wa soka.

Le Bris: Arsenal Ndio Timu Bora Ulaya Kwa SasaLe Bris pia ameonya dhidi ya Sunderland kujikita zaidi kwenye ulinzi, akiamini mbinu hiyo inaweza kuwa na madhara wanapokutana na timu kubwa kama Arsenal. Kocha huyo anataka vijana wake waonyeshe ujasiri na kutumia nafasi watakazopata ili kujaribu kupata matokeo mazuri mbele ya mashabiki wao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.