Robert Lewandowski ameanza kutoa ishara kubwa kwamba safari yake ndani ya Barcelona inaweza kuwa inaelekea mwisho. Baada ya kusherehekea ubingwa mwingine wa La Liga na Barca, mshambuliaji huyo wa Poland amekiri kuwa anafikiria kuhamia ligi zisizo na presha kubwa ili kufurahia zaidi maisha na soka katika hatua za mwisho za kazi yake.

Akizungumza wakati wa sherehe za ubingwa baada ya ushindi dhidi ya Real Madrid, Lewandowski alisema wazi kuwa bado hajafanya uamuzi wa mwisho kuhusu mustakabali wake. Nyota huyo mwenye karibu miaka 38 amesema bado anajisikia vizuri kimwili, lakini anatambua kuwa muda umefika wa kuanza kufikiria mazingira yenye ushindani mdogo zaidi.
Kauli hiyo imeongeza nguvu kwenye tetesi zinazomuhusisha na kuhamia Marekani, hasa klabu ya Chicago Fire ya MLS. Lewandowski amesema yuko tayari kusikiliza ofa mbalimbali kabla ya kufanya maamuzi, huku akifichua kuwa amebakiwa na siku 51 tu kwenye mkataba wake wa sasa Barcelona.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Pamoja na hali hiyo ya sintofahamu, mshambuliaji huyo ameonyesha fahari kubwa kwa mafanikio aliyoyapata katika maisha yake ya soka. Amesema ametwaa jumla ya mataji 14 ya ligi akiwa na klabu tofauti, jambo ambalo linampa heshima kubwa binafsi na kitaaluma. Kwa Lewandowski, ushindi umekuwa sehemu ya maisha yake kwa miaka mingi.

Wakati wengine wakianza kumshauri astaafu, Lewandowski ameweka wazi kuwa bado hana mpango wa kuacha soka. Akimjibu kwa utani mwenzake Szczesny aliyependekeza afikirie maisha baada ya soka, mshambuliaji huyo alisema bado ana nguvu, ana furaha na bado ana kiu ya kuendelea kucheza.



