Mshambuliaji wa FC Barcelona, Robert Lewandowski, ameandika historia mpya katika michuano ya UEFA Champions League baada ya kufunga dhidi ya timu 41 tofauti.
Kwa mafanikio hayo, Lewandowski amemzidi nyota wa zamani wa FC Barcelona, Lionel Messi, ambaye aliwahi kushikilia rekodi hiyo kwa kufunga dhidi ya timu 40 tofauti katika mashindano hayo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Rekodi hiyo inamweka Lewandowski kuwa mchezaji pekee aliyewahi kufunga dhidi ya idadi kubwa zaidi ya timu katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, jambo linalothibitisha uimara na ubora wake wa muda mrefu katika soka la kiwango cha juu.
Katika mafanikio hayo, mshambuliaji huyo raia wa Poland amefunga mabao dhidi ya timu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo England, Hispania, Italia, Ujerumani, Ufaransa, Ureno na Uholanzi, pamoja na nchi nyingine nyingi za Ulaya.
Uwezo huo unaonyesha uimara wake katika mazingira tofauti ya ushindani, huku Lewandowski akiendelea kujiweka miongoni mwa washambuliaji bora zaidi kuwahi kutokea katika historia ya soka duniani.

