Mchezaji Roberto Lewandowski wa klabu ya Fc Barcelona ameendelea kudhihirisha ubora wake kila uchawao kunako ligi kuu ya Hispania maarufu kama La liga.

Mchezaji huyo ambae amejiunga na klabu hiyo akitokea kwa mabingwa wa Ujerumani klabu ya Fc Bayern Munich katika majira haya ya joto amekua na kiwango bora sana tangu kujiunga klabuni hapo.

lewandowskiLewandowski amefanikiwa kuweka kimiani mabao mawili kati ya matatu yalioiwezesha klabu hiyo kupata ushindi wa tatu kwa bila dhidi ya klabu ya Elche na kufikisha jumla ya magoli tisa katika michezo sita aliyoitumikia timu kwenyer ligi kuu nchini Hispania.

Barcelona wanakwenda kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada kucheza michezo sita ya ligi hiyo na kukusanya jumla ya alama kumi na sita huku Roberto akiwa miongoni mwa wachezaji wanaoisaidia timu hiyo kwa kiwango kikubwa mpaka kufikia ilipo kwasasa ndani ya msimu huu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa