Robert Lewandowski anajiandaa kusaini mkataba wa miaka minne na klabu ya Barcelona kwa dau linaloelezwa kufika euro milioni 50.

Uvumi wa kwamba Lewandowski atajiunga na Barca ulianza kabla hata ya msimu uliisha kufika tamati lakini sasa imethhibitika kwamba nyota huyo wa Poland anajiunga na timu ya Xavi Hernandez ikiwa ni mwaka mmoja tangu Messi kuihama The Blaugrana.

Taarifa kutoka kwa klabu hiyo ilisema: “FC Barcelona na Bayern Munich wamefikia makubaliano kimsingi juu ya uhamisho wa Robert Lewandowski, ikitegemea mchezaji huyo kufaulu vipimo vya afya na mikataba kusainiwa.”

Lewandowski anaachana na Bayern Munich akiwa ameifungia Bayern mabao 344 katika michezo 375 kwenye mashindano yote.

Siku ya Jumamosi Lewandowski alikuwa akiwaaga mashabiki wa Bayern Munich kupitia mtandao wa Instagram akiandika: “Ningependa kuwashukuru wachezaji wenzangu, wafanyakazi, usimamizi wa kilabu na kila mtu ambaye amekuwa akiniunga mkono kila wakati na kutuwezesha kushinda mataji kwa FC Bayern,”


BASHIRI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa