Liam Rosenior Amtetea Jorgensen Baada ya Chelsea Kuchapwa 5-2 na PSG

Kocha wa Chelsea FC, Liam Rosenior, amemtetea kipa Filip Jørgensen licha ya kufanya kosa lililosababisha timu hiyo kupoteza mabao 5-2 dhidi ya Paris Saint-Germain katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League uliochezwa Jumatano. Kosa la Jørgensen lilitokea dakika ya 74 baada ya pasi yake kukatwa na kupelekea kiungo Vitinha kufunga bao la tatu kwa PSG.

Liam Rosenior Amtetea Jorgensen Baada ya Chelsea Kuchapwa 5-2 na PSGRosenior alisema makosa ni sehemu ya mchezo wa mpira wa miguu na hayapaswi kumlenga mchezaji mmoja. “Wachezaji hufanya makosa na Filip si wa kwanza kufanya hivyo. Ni sehemu ya soka, lakini ni matokeo yanayoumiza,” alisema kocha huyo akizungumzia tukio hilo lililoibadilisha mechi.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika mchezo huo, Chelsea FC walifanikiwa kusawazisha mara mbili kupitia mabao ya Malo Gusto na Enzo Fernández baada ya Paris Saint-Germain kuongoza kupitia Bradley Barcola na Ousmane Dembélé. Hata hivyo, dakika za mwisho za mchezo ziligeuka kuwa ngumu kwa Chelsea na kuruhusu wapinzani wao kuongeza mabao zaidi.

Liam Rosenior Amtetea Jorgensen Baada ya Chelsea Kuchapwa 5-2 na PSG

Kocha Rosenior alikiri kuwa dakika 15 hadi 20 za mwisho zilikuwa na makosa mengi yaliyoiathiri timu yake. “Ni matokeo ya kukatisha tamaa kwa sababu kwa muda mwingi wa mchezo nilifurahishwa na kiwango cha timu. Lakini dakika za mwisho zilikuwa za ajabu na hilo ni jukumu langu. Tulikosa utulivu na timu nzuri kama PSG ilituadhibu,”

Uamuzi wa kumuanza Jørgensen badala ya kipa Robert Sánchez sasa unatarajiwa kujadiliwa zaidi, hasa ikizingatiwa kwamba kipa huyo wa Denmark alikuwa akicheza mchezo wake wa tatu tu wa UEFA Champions League msimu huu. Rosenior alieleza kuwa kila kipa ana ubora wake.

“Rob ni mzuri sana katika mipira ya juu na kuokoa mashuti, lakini Filip ana ubora wa kutuliza mchezo akiwa na mpira, jambo lililotusaidia katika baadhi ya mechi.”

Kwa upande wa Paris Saint-Germain, kocha Luis Enrique alisema ushindi huo ni muhimu huku wakijiandaa na mchezo wa marudiano.

 “Tulijaribu kuendelea kucheza dhidi ya timu yenye nguvu na ubora wa kiufundi. Tunahitaji kuendelea na pia kupata mapumziko ili kujiandaa na mchezo wa pili,” alisema Enrique, akisisitiza kuwa timu yake bado inaendelea kutafuta kiwango bora kilichowapa ubingwa wa Ulaya msimu uliopita.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.