Klabu ya Liverpool wanaandaa mkataba wa mchezaji pamoja na pesa kwa ajili ya Jude Bellingham huku wakijaribu kushinda katika kinyang’anyiro cha kuwania saini yake.

Liverpool Kumtoa Keita na Pesa Kwaajili ya Bellingham

Liverpool wako tayari kumpeleka Naby Keita Borussia Dortmund pamoja na kiasi kikubwa cha pesa ili kukamilisha dili hilo Januari. Maonyesho ya Bellingham kwa BVB na England yanamaanisha kuwa hisa yake inaendelea kupanda kama vipaji vya vijana wa Uropa.

Sasa jarida la Ujerumani BILD linaamini kuwa  Jurgen Klopp ataharakisha mipango yake ya kuhakikisha wanampata mchezaji huyo kutokana na kuwa na uhitaji nae mkubwa sana, pia mchezaji huyo na kiwango cha kuvutia kwasasa.

Ilionekana kuwa kikosi hicho cha Anfield kilikuwa kikipewa nafasi kubwa ya kumsaini Bellingham msimu ujao wa joto huku wakitafuta kuimarisha safu yao ya kiungo,  lakini Marca wanasema kuwa Real Madrid wamemfanya kuwa shabaha yao kuu na wana pesa za ziada, bila kutarajia kwamba watamfuatilia tena Kylian Mbappe.

 

Liverpool Kumtoa Keita na Pesa Kwaajili ya Bellingham

Pamoja na hayo Manchester United wamekuwa na nia ya muda mrefu ya kumnunua kiungo huyo wa zamani wa Birmingham, huku ripoti zikisema Manchester City walihisi kuwa walikuwa mbele ya foleni ya kumtaka kiungo huyo.

Lakini mpaka sasa Liverpool ambayo ipo chini ya kocha mkuu Jurgen Klopp wanaamini kwamba kwa kumpeleka Keita pamoja pesa  Dortmund  inamaanisha wanaweza kupata makubaliano juu ya dili hilo, ambapo kama Jude akifanya vizuri zaidi kwenye Kombe la Dunia bei yake sokoni itaongezeka zaidi.

 

Liverpool Kumtoa Keita na Pesa Kwaajili ya Bellingham

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa