Shabiki wa klabu ya Liverpool amenunua basi ya bei rahisi nchini Uingereza ili aweze kubeba mashabiki wenzie kwenda kuangalia mchezo wa fainali kati ya klabu ya Liverpool dhidi ya Real Madrid nchini Ufaransa kwenye jiji la Paris.
Klabu ya Liverpool inakwenda kumkabili klabu ya Real Madrid ambay ni bingwa wa hispania ili kwenda kuchukua kombe lake ka saba la ligi ya mabingwa ulaya, huku wakiwa na tiketi 20,000 kwa ajiri ya mchezo huo lakini iadadi ya mashabiki inatarajiwa kuwa kubwa zaidi watao safiri kwa ajiri ya mchezo huo.
Kutokana na uhitaji kuwa mkubwa wa usafiri na kupelekea nauli kupanda, huku baadhi ya mashabiki wakilipisha zaidi kwa ajiri ya tiketi za ndege na vivuko kwa ajiri kusafiri kwenda nchini Ufaransa, Shabiki wa Liverpool simon Wilson amenunua basi laku na atawaendesha baadhi ya mashabiki mpaka jijini Paris.
Simon Wilson atawalipisha mashabiki wenzie kiasi cha  £1 tu kwenda kuangalia mchezo huo, japokuwa basi hilo litatumia gharama zaidi ambapo yeye ndio atazibeba.
Miliki wa chanel ya Youtube ambae aliongeza watazamaji 950,000 kwenye mtandao huo wa kijamii, alinunua gari la  £40 mwaka 2019 kumbeba rafiki yake kwenda kuangalia mchezo wa fainali ambapo liverpool walifanikiwa kushinda kwenye mchezo huo wa fainali dhidi ya Tottenham.
“Miaka kadhaa iliyopita niliona mashabiki wengi wakilipisha zaidi, mashabiki wengi walishinda kwenda wambao walikuwa wanataka kwenda kwa sababu ilikuwa gharama kubwa. Wilson alilimbia Liverpool ECHO.
“Kwa fainali hii, nilikuwa nakwenda kutumia Skoda lakini kuna siti chache ndani ya gari. Na tulikuwa tunataka kitu kikubwa kidogo ili kuweza kuwasaidia watu, ndipo nikanunua basi la bei ya chini ambalo nilifanikiwa kupata.
“Nilikuwa natafuta basi la bei chee kwenye mtandao wa google hili ndilo likaja.”
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.