Klabu ya Liverpool imemtambulisha rasmi beki wa kati mwenye umri wa miaka 20, Jeremy Jacquet, kama usajili mpya kuelekea msimu wa 2026/27. Mfaransa huyo ametua Anfield akitokea Rennes kwa ada ya euro milioni 64, huku euro milioni 6 zikitarajiwa kulipwa kama nyongeza kulingana na mafanikio yatakayofikiwa. Usajili huo ulikuwa umekamilika tangu mwezi Februari lakini umetambulishwa rasmi sasa.
Liverpool imemleta Jacquet kama mbadala wa beki Ibrahima Konaté, ambaye ameondoka baada ya kumalizika kwa mkataba wake na kujiunga na Real Madrid bila ada ya uhamisho. Jacquet amekuwa akitajwa kama mmoja wa mabeki chipukizi wenye uwezo mkubwa nchini Ufaransa baada ya kukulia katika akademi ya Rennes na kuingia kikosi cha kwanza msimu wa 2023/24.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kabla ya kujihakikishia nafasi Rennes, Jacquet alitumia msimu mmoja na nusu kwa mkopo katika klabu ya Clermont, ambako alipata uzoefu mkubwa. Msimu uliopita alicheza mechi 21 kabla ya kukumbwa na jeraha la bega mnamo Februari 7, lililomlazimu kufanyiwa upasuaji na kumaliza msimu mapema.
Akizungumza baada ya kutambulishwa, Jacquet alisema kujiunga na Liverpool ni ndoto iliyotimia. “Nina furaha sana. Nilipoona miundombinu ya klabu hii nilijiona tayari kuwa sehemu yake. Najisikia vizuri hapa na nina hamu kubwa ya kuanza safari yangu mpya,” alisema beki huyo wa Kifaransa.
Jacquet aliongeza kuwa, “Kwangu hii ni ndoto kubwa kwa sababu Liverpool ni moja ya vilabu vikubwa duniani. Ni heshima kubwa kuwa hapa.” Hadi sasa bado hajatangazwa jezi namba atakayovaa, huku akitarajiwa kufanya kazi chini ya kocha mpya Andoni Iraola. Mbali na Jacquet, Liverpool pia imethibitisha usajili wa winga Mhispania Víctor Muñoz kutoka Osasuna kuelekea msimu mpya.


