Kocha wa Colombia Néstor Lorenzo ametoa onyo kwa kikosi chake kutokuwa na kiburi kabla ya mchezo wao wa Kombe la Dunia dhidi ya Uzbekistan, akisema mashindano hayo yameonyesha hakuna timu rahisi. Colombia wanarejea katika mashindano hayo makubwa baada ya kukosa fainali za 2022.
Lorenzo amesema: “michuano ya Dunia inatuonyesha kuwa hakuna timu ndogo na hakuna anayepaswa kudharauliwa.” Ameongeza kuwa Uzbekistan ni timu yenye nidhamu, kocha mzuri na wachezaji wenye vipaji ambao wanaweza kuleta changamoto kubwa uwanjani.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha huyo amesema Colombia wamejiandaa vizuri kutokana na mwenendo mzuri wa mechi za mchujo, huku wakitegemea nyota wao kama Luis Díaz pamoja na nahodha James Rodríguez. Ameeleza kuwa Rodríguez ameendelea kuboresha hali yake ya afya na bado ana mchango mkubwa kwenye timu.
Amesema: “James anaendelea vizuri na hali yake ya mwili inaimarika. Kipaji chake kinampa uwezo wa kuamua matukio muhimu hata kama hatakimbia sana kama wengine.” Lorenzo pia amekataa dhana kuwa Colombia inaweza kushindwa kushindana na timu zenye kasi na nguvu kubwa.
Akihitimisha, Lorenzo amewashukuru mashabiki zaidi ya 65,000 wanaotarajiwa kuisapoti Colombia Mexico City, akisema wanataka kuwapa furaha kwa kurejea kwaomichuano ya Dunia. Amesema: “Colombia ni furaha, tunataka kucheza vizuri na kuwapa watu sababu ya kutabasamu.”


