Paris Saint-Germain wanajiandaa kwa mchezo muhimu wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Bayern Munich, huku kocha Luis Enrique akitumia kumbukumbu nzuri za uwanja wa Allianz Arena kuongeza motisha kwa kikosi chake.
PSG wanaingia katika mchezo huo wakiwa mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-4 baada ya ushindi wa kusisimua kwenye mkondo wa kwanza nyumbani, lakini wanajua changamoto kubwa inayowasubiri nchini Ujerumani. Luis Enrique alisema “Tuna kumbukumbu nzuri sana hapa Munich. Kurudi hapa ni furaha kubwa kwa sababu tunakumbuka tulichokipitia msimu uliopita.”
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha huyo alikumbusha pia mafanikio yake ya zamani akiwa na FC Barcelona alipoifunga Bayern katika hatua ya nusu fainali, akisema “Tulicheza hapa pia tukiwa Barcelona na tukafanikiwa kufika fainali na hatimaye kushinda ubingwa. Hivyo hii ni motisha kubwa kwangu.”
Katika mkondo wa kwanza uliokuwa na mabao mengi, PSG waliongoza 5-2 kabla ya Bayern kurudisha presha na kufunga mabao mawili ya karibu, jambo linaloifanya mechi ya marudiano kuwa ngumu kutabiri. Luis Enrique alisema “Hatutarajii mchezo tofauti sana na ule wa kwanza. Kila timu inaamini inaweza kushinda.”
Kocha huyo alisisitiza kuwa PSG hawataingia kucheza kwa kujilinda licha ya kuwa na faida ya bao moja. Alisema “Lengo letu ni kushinda kila mchezo. Hatuko hapa kulinda matokeo, bali kushambulia na kushinda.”
PSG wanategemea kuendeleza kasi yao ya ufungaji mabao huku Bayern wakitafuta kurudi kwa nguvu mbele ya mashabiki wao. Mshindi wa jumla atatinga fainali ya UEFA Champions League itakayochezwa Budapest, Hungary.


