UONGOZI wa klabu ya Simba umefikia makubaliano na Charles Ayeikoh Lukula kuwa kocha Mkuu wa kikosi cha Simba Queens.

Kabla ya kujiunga na Simba, Kocha huyo alikuwa akifundisha kikosi cha She Corparate ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu nchini Uganda kwa msimu uliopita.

Lukula ametangazwa leo na klabu ya Simba kuwa kocha Mkuu kwa mkataba wa miaka miwili.

Kocha huyo ana leseni A ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambayo inamuwezesha kukiongoza kikosi cha Simba Queens kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itafanyika nchini Morroco.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa