Mac Allister: England Hawana Kasi Kama Timu za EPL Katika Michuano ya Dunia

Kiungo wa Argentina na Liverpool, Alexis Mac Allister, amesema England ni timu yenye ubora mkubwa lakini haijaonyesha kasi ileile anayokutana nayo kila wiki kwenye Ligi Kuu England, kuelekea mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Dunia 2026. Argentina na England zinatarajiwa kukutana katika mchezo wenye historia kubwa kwenye michuano hiyo.

Mac Allister: England Hawana Kasi Kama Timu za EPL Katika Michuano ya DuniaMac Allister, ambaye anafahamu vyema uwezo wa wachezaji wengi wa England kutokana na kucheza nao kwenye Ligi Kuu England, alisema amegundua tofauti ya kiwango cha kasi na nguvu ya kimwili katika mashindano haya. “Ninacheza dhidi yao kila wiki na ni wazi kuwa wana nguvu kubwa kimwili. Lakini katika michuano hii ya Dunia sijaona kasi ile inayowatambulisha kwenye Ligi Kuu England. Sijui kama ni kutokana na uchovu, joto au sababu nyingine,” alisema kiungo huyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Mchezaji huyo pia alizungumzia historia ya Argentina dhidi ya England, hasa kumbukumbu ya mwaka 1986 ambapo Diego Maradona alifunga bao maarufu la “Hand of God” na lile la “Goal of the Century” katika ushindi wa mabao 2-1. Mac Allister alisema matukio hayo bado yanawapa hamasa wachezaji wa sasa, ingawa ni vigumu kufikia kiwango cha Maradona.

Mac Allister: England Hawana Kasi Kama Timu za EPL Katika Michuano ya Dunia“Ni vigumu kupata msukumo kutoka kile alichofanya Diego kwa sababu karibu haiwezekani kufanya mambo aliyofanya uwanjani. Ni Leo Messi pekee ambaye anaweza kufanya mambo ya aina hiyo. Tunapoona video za Diego na mchezo wa mwaka 1986 kwenye mitandao ya kijamii, tunapata nguvu na tunakumbuka umuhimu wake kwa nchi yetu,” alisema Mac Allister.

Mac Allister: England Hawana Kasi Kama Timu za EPL Katika Michuano ya DuniaAkizungumzia nafasi ya Argentina kama mabingwa watetezi wa dunia, kiungo huyo alisema uzoefu wao ni faida lakini hautoshi kuhakikisha ushindi. “Kuwa na uzoefu wa kushinda michuano ya Dunia ni jambo zuri, lakini hakuhakikishi chochote. England wana wachezaji wenye ubora mkubwa ambao pia wamezoea kucheza mechi kubwa na mazingira kama haya,” aliongeza.

Mac Allister: England Hawana Kasi Kama Timu za EPL Katika Michuano ya DuniaMac Allister alimalizia kwa kusema Argentina itaendelea kuamini mfumo wao licha ya kuheshimu uwezo wa England. “Ni wazi kuwa England ni timu kubwa na tunawaheshimu sana, lakini sisi tunaamini katika kile tunachofanya. Hatutabadilisha utambulisho wetu kwa sababu ya mpinzani yeyote,” alisema kiungo huyo kabla ya pambano hilo la nusu fainali.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.