Nahodha wa Algeria na winga nyota, Riyad Mahrez ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Algeria, akihitimisha safari yake ya muda mrefu iliyojaa mafanikio makubwa katika soka la kimataifa.
Mahrez amechukua uamuzi huo kufuatia Algeria kuondolewa kwenye michuano ya Dunia 2026 katika hatua ya 32 bora baada ya kufungwa mabao 2-0 na Uswisi, matokeo yaliyoweka mwisho wa safari ya mashindano ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 35.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza baada ya kutangaza uamuzi huo, Mahrez alisema: “Nimeipigania nchi yangu kwa moyo wangu wote. Ni wakati wa kizazi kipya kuchukua nafasi na kuendeleza safari hii.” Ameongeza pia kuwashukuru mashabiki, makocha na wachezaji wenzake kwa sapoti waliompa katika maisha yake ya timu ya taifa.
Katika kipindi chote cha kuitumikia Algeria, Mahrez amecheza michezo 119, akifunga mabao 40 na kutoa pasi za mabao 45, takwimu zinazomweka miongoni mwa wachezaji bora na wenye mchango mkubwa zaidi katika historia ya soka la nchi hiyo.
Mafanikio yake makubwa zaidi ni kuiongoza Algeria kutwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2019 akiwa nahodha, mafanikio yaliyoweka historia mpya kwa taifa hilo na kumfanya kuwa mmoja wa wachezaji waliowahi kuacha alama kubwa zaidi katika soka la Algeria.


