Majeraha ya Wachezaji Yampasua Kichwa Tuchel.

Mapambano ya kuwa fit kwa Kylian Mbappe yana mpasua kichwa Thomas Tuchel kuelekea mchezo wa Paris Saint-Germain wa Ligue 1 dhidi ya Strasbourg siku ya Jumatano.
Majeraha ya Wachezaji Yampasua Kichwa Tuchel.
Mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe.

Mshambuliaji huyo mwenye kasi wa Ufaransa amekuwa akipambana sana na majeraha katika mguu wake wa kushoto tangu PSG iliposhinda 2-0 wiki iliyopita na hali yake ya kucheza dhidi ya Strasbourg bado iko mashakani.

Presnel Kimpembe, Layvin Kurzawa (wote wana majeraha ya hamstring) na Alessandro Florenzi (kifundo cha mguu) wameongeza orodha ya majeruhi ya PSG ambayo inakaa wachezaji 10, wakati kukosekana kwa Mbappe kungeifanya iwe 11.

Alipoulizwa katika mkutano wa waandishi wa habari kabla ya mechi jinsi anavyopanga kudhibiti hali hiyo, Kocha Mkuu Tuchel alijibu: “Sijui nifanye nini kesho, bado sijaamua kuwa nani atakayecheza.

“Vijana wengine wako hatarini na majeraha yao, bado sijaamua, bado ninahitaji kuzungumza na daktari kuhusu wachezaji na kusubiri kikao cha mazoezi baadaye.”

Akiwa na idadi kubwa ya upungufu ya wachezaji na dirisha la usajili la Januari lipo karibu sana kufunguliwa, Tuchel aliulizwa kama atakuwa na ulazima wa kuongeza wachezaji ili kuimarisha kikosi.

“Hali iko hivi sasa, hatujui tutafanya nini kwenye dirisha la uhamisho, sijafikiria sana kusema ukweli,” alijibu.

“Jambo muhimu zaidi ni kuwa na majeraha machache. Huo ndio mtazamo wangu sasa hivi.”


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

11 Komentara

    Duu lazi uwe na mawazo mawachezaji kwasababu ware wario namajeraha ndio uwa anaowategemea kwenye kufanya vizuri

    Jibu

    Yatamtesa kweli maana wachezaji minimum wore wamekuja bimeo

    Jibu

    Pole Sana

    Jibu

    Duuuh

    Jibu

    Majeruh yanawakost psg msimu huu

    Jibu

    Majeraha yamezidi kuwa mengi msimu huu PSG yanawakost

    Jibu

    Duu pole sana

    Jibu

    I feel sorry to him

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Hata mie yananipasuaga kichwa sana

    Jibu

Acha ujumbe