Paolo Maldini mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya Ac Milan ameongea kuhusu hatama ya mchezaji wa nyota kikosi Rafael Leao ambae amekua akihusishwa na miamba tofauti tofauti barani ulaya.

Gwiji huyo wa zamani wa klabu hiyo anaamini nyota huyo atasalia klabuni hapo zaidi baada ya kuuonesha kiwango bora katika msimu uliomalizika na Milan kua mabingwa wa Italia huku Leoa akiwa mchezaji bora wa mwaka nchini Italia.

maldiniNyota aliekua anahusishwa na klabu ya Chelsea kwenye dirisha lililopita kutoka na kiwango bora alichokionesha katika klabu hiyo na mazungumzo yamekwama baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 raia wa Ureno lakini Maldini hana wasiwasi na anaamini  Milan ndio mahali sahihi kwa maendeleo ya mchezaji huyo.

“Tayari tumeanza kuongea naye.sio sasa, tangu muda mrefu. unapotaka kumuongezea mchezaji mkataba kuna ugumunmna urahisi ewake na hapo inategemeana na mchezaji mwenyewe lakini matamanio ya klabu ni kuona mchezaji huyo anasasini mkataba mpya” aliliambia gazeti moja nchini italia.

“Suala kumuongezea  mkataba tumeanza miezi mingi iliyopita, ili kuendelea kua bora Rafa anajua anatakiwa kubaki na sisi. Sisi ni klabu changa na inayokua”.

“Bado anatakiwa kujifunza mambo mengi lakini tunakusudia kufanya makubwa na kukua naye”

“Chelsea walituma ofa lakini haikufika rasmi na kikawaida ilikataliwa tu aliongeza kwa kusema Huenda tusiwe tayari kufikiria fainali lakini kuota ndoto ni lazima, Kwasababu Milan ni timu ambayo vigogo wasingependa kukutana nayo”.alimaliza kwa kusema hivo.

 

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa