Man U ni Kilaza au Mteja wa Barca?

Mechi ya mwisho kati ya wababe hawa wawili, kutoka EPL na LA Liga ilikuwa April 16 2019. Ilikuwa ni ya pili kwenye mzunguko wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya United walipokea kichapo cha bao 3 bila. Wakati mechi ya mzunguko wa kwanza pia alipokea kichapo cha bao 1 mtungi.

Nakukumbusha mechi zao zilizobamba zaidi siku zilizopita! Mara ta mwisho United kumchapa Barcelona ilikuwa mwaka 2009.

Man U 2 -1 Barcelona       Mei 15, 1991

Mei 15, 1991 mabingwa hawa walikutana tena kwenye fainali ya Kombe la Washindi wa Vikombe -Cup Winners’ Cup, United walifurukuta kujihakikishia ushindi wa taji ambalo lilikuwa ni taji lao la pili kubwa Ulaya.

Barcelona 4-0 Man U        Novemba 2, 1994

Barcelona walijitolea uvivu kwenye Kundi A la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuhakikisha wana wachapa vyema kabisa wapinzani wao; nyota Stoichkov aliwachapia Barca magoli 2, na mbrazili Romario akicheka na nyavu mara moja pia beki wa kati Albert Ferrer akichapa bao la 4 na kuwaacha Man U wakisepa watupu kabisa!

Man U 0-2 Barcelona        Mei 27, 2009

Ligi ya Mabingwa Ulaya fainali! Hapa United walikuwa wametoka kumchapa Chelsea kama miezi 12 iliyopita kule Moscow, hapa United walikuwa ni timu ya kwanza kujiwekea mazingira mazuri ya kutetea ubingwa lakini wakakwamishwa na vijana wa Pep Guardiola. Samuel Eto’o ndiye aliyewachapia Barcelona bao la ufunguzi ndani ya dakika 10 tu, na Lionel Messi akacheka tena na nyavu kukamilisha mabao 2-0 yaliyokwamisha ndoto ya Man U kutetea ubingwa. Barca wakafanikiwa kunyakua mataji matatu ya Champions League, LaLiga na Copa del Rey.

Barcelona 3-1 Man U        Mei 28, 2011

Hapa messi alipata nafasi ya kuonesha umuhimu wake mkubwa kwa Barcelona ambao waliweza kumshinda mpinzani wao Real Madrid kwenye nusu fainali. Wayne Rooney alijaribu kusawazisha bao lililochapwa na Pedro lakini Messi aliweka mkwaju makini kabisa nyavuni kukamilisha bao 2 kabla David Villa hajamalizia kazi kabisa kukamilisha bao 3-1

Juu ni baadhi, Angalia rekodi ya jumla ya mechi 10 zilizopita hapa chini.

DateMechi MatokeoLigi
07 Mar 1984Barcelona v Manchester United2-0UEFA European Cup Winners Cup
21 Mar 1984Manchester United v Barcelona3-0UEFA European Cup Winners Cup
15 May 1991Barcelona v Manchester United1-2UEFA European Cup Winners Cup
19 Oct 1994Manchester United v Barcelona2-2UEFA Champions League
02 Nov 1994Barcelona v Manchester United4-0UEFA Champions League
16 Sep 1998Manchester United v Barcelona3-3UEFA Champions League
25 Nov 1998Barcelona v Manchester United3-3UEFA Champions League
23 Apr 2008Barcelona v Manchester United0-0UEFA Champions League
29 Apr 2008Manchester United v Barcelona1-0UEFA Champions League
27 May 2009Barcelona v Manchester United2-0UEFA Champions League
28 May 2011Barcelona v Manchester United3-1UEFA Champions League
10 Apr 2019Manchester United v Barcelona0-1UEFA Champions League
16 Apr 2019Barcelona v Manchester United3-0UEFA Champions League

38 Komentara

  duh emu tuachane na history ya hamsini na kutitu huko hii barc ya juzi ndio ilikuwa timu bora zaid duniani kuishuhudia mpaka sasa Ferguson kupata kiharusi alistahili aisee

  Jibu

  Bahati mbaya hapa tumeanza miaka ya 1980’s! Hata tukianza na miaka ya 2000;s Man U bado wana mlima wa kupanda.

  Jibu

  Haha haha haha man u kilaza

  Jibu

  Messi alipata nafasi ya kuonyesha
  Umuhimu wake mkubwa kwa Barcelona ili kumshinda mpinzani wake real Madrid

  Jibu

  Ni timu Bora Barcelona dunian

  Jibu

  Kwa historia hiyo kweli ni kilaza

  Jibu

  Man U jau tu

  Jibu

  Messi alipata nafasi kubwa ya kuonyesha umuhimu wake kwa Barcelona na kuonyesha mpinzani wake real Madrid

  Jibu

  Man u kilaza sio kwa kupigwa huko ila hawa man u wakipigwa mji huwa unatulia sana ila wakishinda watu hatulali wako kama simba

  Jibu

  Mimi ndo mana siwakubaligi man u

  Jibu

  Man U mmeniaibisha kwa kwelii. Alosema kilaza hajakosea hata kidogo

  Jibu

  Tengua kauli Man U so kilaza bana,wameteleza tu

  Jibu

  Walimtesa sana babu Fegi hawa barca

  Jibu

  Man U bado wateja tuu kwa Barca

  Jibu

  hapana man u sio kilaza

  Jibu

  Kwer kila mbabe na mbabe wake ndio apo tunaona ni jinsi gani walivyokuwa wanachezea kipigo cha kutosha

  Jibu

  Kwa wakati ule Barcelona walikuwa vizuri
  Kwa man utd ya sasa hivi Barcelona achomoki#

  Jibu

  Man u bado hajafikia kiwango kizuri kama barca

  Jibu

  Man hana shuhuli

  Jibu

  Mwaka 2011 messi alipata nafasi ya kuonesha umuhimu wake mkubwa kwa Barcelona

  Jibu

  Sio kilaza Bali Kuna wakati Barcelona walikuwa wanabebwa na marefaaa

  Jibu

  Man u vilaza

  Jibu

  Barca ya kipindi iko ilikuwa na vipaji vya hatari sana kuliko man u.

  Jibu

  dah mambo magumu

  Jibu

  United kwa wacatalunya mamb magumu sana thanks meridian bet tz

  Jibu

  Man u siwaelew kabisa asahv wamekuwa wateja wa Kila team

  Jibu

  Man u vilaza

  Jibu

  Man u hawako vizur

  Jibu

  Atari sana huo mtanange

  Jibu

  Dah ata sielewi.

  Jibu

  Mmh man huwa simlewi hayuko vzr kwenye mpira

  Jibu

  Man u jeshii

  Jibu

  Man u kibonde sana yaani kapigwa mpaka bas

  Jibu

  Ni mke wa Barca

  Jibu

  Man u ni jembe

  Jibu

  Duuuh

  Jibu

  Kila mtu na mnyonge wake #Meridianbettz

  Jibu

  Man mteja tu kwa barcelona

  Jibu

Acha ujumbe