Manchester United inaripotiwa kumvizia mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Randal Kolo Muani, baada ya dili lake la kujiunga na Juventus kudorora.

Kwa mujibu wa ripoti, nyota huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26, ambaye alijiunga na PSG mwaka 2023 akitokea Eintracht Frankfurt ya Ujerumani, alikosa nafasi ya kudumu kikosini na alihamishiwa kwa mkopo Juventus mwezi Januari alipomaliza akiwa na mabao 10 katika mechi 22 kwenye mashindano yote.
Hata hivyo, mipango ya kumfanya kuwa mchezaji wa kudumu Turin imekwama kutokana na changamoto za kifedha kwa Juventus, ambao sasa wanalazimika kuuza baadhi ya nyota wao ili kupata fedha za kufanikisha usajili huo.

Taarifa zinasema kuwa PSG hawana mpango wa kumrudisha Muani kikosini, na wako tayari kumuuza moja kwa moja au kumtoa kwa mkopo wenye kipengele cha kumnunua moja kwa moja mwishoni mwa msimu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Mzozo wa bei kati ya PSG na Juventus sasa umeacha mlango wazi kwa United na klabu nyingine zinazomfuatilia Muani, na ikiwa mazungumzo yataenda vizuri, tunaweza kumshuhudia akiwa anavaa jezi nyekundu ya Mashetani Wekundu msimu ujao.


