Klabu ya Manchester City imepanda kileleni mwa Premier League baada ya ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Burnley, ushindi ambao pia umethibitisha rasmi kushuka daraja kwa Burnley kuelekea Championship.
Mchezo ulianza kwa kasi kubwa ambapo Rayan Cherki alikaribia kufunga mapema kabisa lakini shuti lake liligonga mwamba, kabla ya Erling Haaland kufunga bao pekee la mchezo baada ya pasi safi ya Jérémy Doku, akiipa City uongozi mapema.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Burnley walijaribu kurudi mchezoni kupitia Quilindschy Hartman na Zian Flemming, lakini walikosa umakini mbele ya lango, hali iliyowaumiza zaidi katika juhudi zao za kusawazisha.
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola alisema “Tulijua mchezo utakuwa mgumu licha ya Burnley kushuka daraja. Lengo letu ni kushinda kila mchezo na kubaki kileleni.”
Katika kipindi cha pili, City walizidi kushambulia kupitia Bernardo Silva na Cherki, lakini kipa wa Burnley Martin Dúbravka alifanya kazi kubwa kuokoa mabao zaidi na kuzuia ushindani kuwa mkubwa.
Guardiola aliongeza “Hatukucheza kwa kiwango chetu bora kwenye kipindi cha pili, lakini muhimu ni pointi tatu. Sasa tunalenga michezo ijayo ya mwisho wa msimu.”
Kwa ushindi huo, Manchester City sasa wanashika nafasi ya kwanza ligi, huku Burnley wakithibitishwa kushuka daraja baada ya msimu mgumu uliowaona wakishinda mchezo mmoja pekee kati ya 25 za mwisho.


