Klabu ya Manchester United ina nafasi ya kujiuliza leo katima michuano ya Carabao pale watakapokutana na klabu ya Aston Villa ambao waliwafunga kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza wikiendi iliomalizika.

Klabu ya Aston Villa ilikatisha rekodi ya Manchester United ya kucheza michezo tisa bila kupoteza kwenye michezo yote baada ya kuwafunga mabao matatu kwa moja katika dimba la Villa Park, Lakini leo United watakua na nafasi ya kulipiza kisasi wakiwa katika dimba la Old Trafford.manchester UnitedMchezo huo ambao utakua wa pili kwa mwalimu Unai Emery ambapo mchezo wa kwanza pia ulikua dhidi ya Man United na kufanikiwa kuwafunga, Hivo leo ana mtihani wa kuendeleza alipoishia katika mchezo uliomalizika wikiendi iliyopita.

Manchester United wao watahakikisha wanapambana wanalipiza kisasi na kufuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo, Kwani wakikubali kufungwa leo ina maana wamekubali kuachia kombe moja kati ya manne ambayo wanashiriki msimu huumanchester unitedIkiwa Man United watashindwa kupata matokeo chanya katika mchezo wa leo basi ina maana watakua wamekubali kua wateja wa Aston Villa kwenye mechi mbili mfululizo, Kitu ambacho kimetokea miaka mingi iliyopita kwa Man United kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Aston villa.JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa