Manchester United Kuongeza Kocha Mwingine

Klabu ya Manchester United ipo kwenye mkakati wa kuboresha benchi la ufundi la klabu hivo kwasasa wako kwenye mpango wa kuongeza makocha wawili kwenye benchi lao.

Klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na gwiji wa zamani wa klabu hiyo Ruud Van Nistelrooy ambaye wanamuhitaji kwajili ya kwenda kuungana na kocha Erik Ten Hag kwenye kikosi hicho msimu ujao, Ambapo wanaamini anweza kuongeza ubora ndani ya kikosi hicho msimu ujao.

manchester united

Wakati mazungumzo yakiendelea na Van Nistelrooy ambayo yanaelezwa yako mbioni kukamilika lakini klabu ya Manchester United inafanya mazungumzo na kocha wa Go Ahead Eagles ya nchini Uholanzi Rene Hake, Jambo ambalo linaonesha namna ambavyo klabu hiyo inataka kuboresha timu hiyo kuanzia kwenye benchi lao la ufundi.

Dili la Van Nistelrooy na Rene Hake likikamilika ina maana Manchester United watakua wameongeza makocha wawili kwenye benchi lake la ufundi, Ambapo makocha watakua wanne kwenye benchi la klabu hiyo huku kuanzia kocha mkuu watakua ni makocha wenye asili ya Uholanzi.

Acha ujumbe