MANCHESTER UNITED wamesema kuwa mechi yao ya dhidi ya FC Sheriff itachezwa kama ambavyo ilipangwa, mechi hiyo ilipangwa kuchezwa Alhamis ya tarehe 15/09/2022 katika Jiji la Moldova.

Taarifa rasmi kutoka klabuni hapo ilisema kuwa, “Kufuatia majadiliano na mabaraza husika ya uongozi na kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa na Serikali ya Uingereza, tunaweza kuthibitisha mechi yetu ya UEFA-Europa League dhidi ya FC Sheriff itafanyika kama ilivyopangwa Alhamisi jioni huko Moldova”.

Manchester United Watakipiga na FC Sheriff

Pia, Mipango ya mechi itasalia vile vile kwa mashabiki wanaosafiri kwenda kuisapoti timu huko Chisinau.

Manchester walianza vibaya mashindano hayo kwa kichapo cha goli 1 dhidi ya Real Sociedad ya Hispania, hivyo hii ni karata ya pili kwa Manchester United kurejesha matumaini ya kufuzu katika hatua inayofuata.

Manchester United Watakipiga na FC Sheriff

Kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II, aliyefariki dunia siku ya Alhamis tarehe 8/09/2022, kulipelekea michezo yote ya timu za uingereza kusitishwa kwa muda kwanza ili kupisha maombolezo wa msiba huo kitaifa. Mamlaka nchini humo zilisema kuwa mchezo yote ya wikiendi iliyopangwa kuchezwa itasitishwa na kupangiwa ratiba upya.

Manchester United Watakipiga na FC Sheriff

Malkia Elizabeth II alizaliwa Aprili 21, 1926 Bruton, London na Kufariki mwaka 2022 akiwa na umri wa miaka 96.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa