Manchester United Yaingia Kwenye Vita ya Kumsaka Rafael Leão

Manchester United imeweka rasmi jina la winga wa AC Milan na timu ya taifa ya Ureno, Rafael Leão, katika orodha yake ya wachezaji wanaowahitaji kuelekea msimu ujao wa usajili.

Manchester United Yaingia Kwenye Vita ya Kumsaka Rafael LeãoKwa mujibu wa ripoti mbalimbali za vyombo vya habari, Leão anaweza kupatikana kwa ada ya chini zaidi kufuatia AC Milan kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, jambo ambalo limefungua milango kwa klabu kadhaa kubwa Ulaya kuanza mazungumzo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Hata hivyo, changamoto kubwa katika dili hilo inatajwa kuwa mshahara wake, ambapo anataka zaidi ya pauni 200,000 kwa wiki, hali inayoweza kuleta mvutano katika mazungumzo ya usajili.

Manchester United Yaingia Kwenye Vita ya Kumsaka Rafael Leão
Inaelezwa kuwa klabu kadhaa ikiwemo Inter Milan, Manchester City, Real Madrid na Atletico Madrid zimeanza mawasiliano ya awali kupitia mawakala wake ili kuhakikisha zinapata nafasi ya kumnasa nyota huyo mwenye uwezo mkubwa wa kushambulia.

Manchester United Yaingia Kwenye Vita ya Kumsaka Rafael LeãoLeão, ambaye kwa sasa yupo Marekani akiwa na timu ya taifa ya Ureno, ameripotiwa kunukuliwa akisema “Ninatafuta changamoto mpya katika klabu yenye malengo ya kushinda mataji makubwa ya Ulaya,” kauli ambayo imezidi kuchochea vita ya usajili kati ya vigogo wa soka la Ulaya. Mkataba wake na AC Milan unaendelea hadi Juni 30, 2028, lakini mustakabali wake unatarajiwa kuwa gumzo kubwa katika dirisha lijalo la usajili.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.