Manchester United imeamua kusitisha kwa muda mazungumzo ya kuongeza mkataba wa nahodha wake, Bruno Fernandes, huku uongozi wa klabu ukielekeza nguvu zake katika mipango ya usajili wa wachezaji wapya kwa ajili ya kuimarisha kikosi kabla ya msimu mpya kuanza.
Kiungo huyo raia wa Ureno kwa sasa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa, ingawa mkataba huo una kipengele kinachoiruhusu klabu kuongeza mwaka mmoja zaidi. Hali hiyo imeifanya Manchester United kutokuwa na haraka ya kukamilisha mazungumzo mapya kwa wakati huu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Vyanzo vya karibu na klabu hiyo vinaeleza kuwa viongozi wa United wana imani kubwa kwamba Fernandes ataendelea kubaki Old Trafford kwa muda mrefu. “Hakuna hofu kuhusu mustakabali wa Bruno kwa sasa, klabu inaamini ataendelea kuwa sehemu muhimu ya mradi wao,” chanzo kimoja kimekaririwa kikisema.
Katika kipindi hiki, Manchester United imeweka mkazo zaidi kwenye soko la usajili huku ikitafuta kuleta sura mpya zitakazosaidia kuimarisha kikosi baada ya msimu uliopita wenye changamoto nyingi. Maboresho katika maeneo kadhaa ya kikosi yanaonekana kuwa kipaumbele kikubwa kwa uongozi.
Inaelezwa kuwa mmiliki mwenza wa klabu hiyo, Jim Ratcliffe, ndiye aliyeweka mkazo mkubwa kwenye usajili mpya, akiamini kuwa kuimarisha kikosi ni jambo la haraka zaidi kwa sasa. “Kipaumbele ni kuleta wachezaji watakaoipeleka timu katika kiwango cha juu zaidi,” zimeeleza taarifa zinazohusishwa na mipango ya klabu hiyo.


