KIPA wa Simba, Aishi Manula amefunguka kuwa kwa msimu huu mambo yamekuwa magumu lakini amefurahi tuzo hiyo kuchukuliwa na kipa wa timu nyingine.
Aishi amesema hayo kwenye usiku wa tuzo za Shirikisho la Soka nchini ‘NBC TFF AWARDS 2022, ‘ zinazofanyika leo alhamis kwenye hoteli ya Johari Rotana, Dar.

“Msimu huu haukuwa mzuri kwangu lakini mimi huwa nafurahi kama kipa mwingine anachukua tuzo kwani hiyo inanifanya najifunza mambo mengi.
“Kwa msimu huu nipo nafasi ya tatu kwenye idadi ya makipa wenye Cleen sheet ila waliopo juu yangu wamekuwa bora sana na wameisaidia timu yao.”