Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford, anatarajiwa kujiunga na kikosi cha timu hiyo katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya nchini Ireland kuelekea kampeni ya Ligi Kuu England 2026/27. Rashford atarejea kambini baada ya kumaliza mapumziko ya lazima kufuatia ushiriki wake na timu ya taifa ya England katika mashindano ya Dunia 2026.
Manchester United itaanza ratiba yake ya maandalizi kwa mchezo dhidi ya Rosenborg nchini Norway Julai 24, kabla ya kusafiri kwenda Sweden kucheza dhidi ya Atlético Madrid na Paris Saint-Germain. Baadaye, kikosi hicho kitaweka kambi ya siku sita nchini Ireland, ambapo kitamalizia maandalizi kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Leeds United utakaochezwa Agosti 12 katika Uwanja wa Croke Park.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa sasa, hatma ya Rashford ndani ya Manchester United bado haijaeleweka baada ya Barcelona kuamua kutotumia kipengele cha kumnunua moja kwa moja kufuatia kipindi chake cha mkopo. Aidha, hakuna klabu iliyotumia kipengele cha pauni milioni 40 kilichoruhusu uhamisho wake ndani ya Ligi Kuu England kabla ya muda wake kuisha mapema mwezi Julai.
“Rashford yupo tayari kufanya kazi chini ya Michael Carrick ikiwa hatafanikiwa kupata uhamisho katika dirisha hili la usajili,” zilisema taarifa zinazoizunguka klabu hiyo. Hali hiyo inaashiria kuwa mshambuliaji huyo yuko tayari kurejesha nafasi yake kikosini licha ya uhusiano wake uliokuwa na sintofahamu na aliyekuwa kocha Ruben Amorim.
Ingawa Rashford anatarajiwa kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya msimu mpya, bado haijafahamika kama atakuwa sehemu ya kikosi cha Manchester United kitakachoanza rasmi msimu wa 2026/27. Mustakabali wake unaendelea kuwa gumzo huku dirisha la usajili likiendelea.


