Marsch Aipa Canada Moyo Kabla ya Mechi ya Ufunguzi wa Michuano Mikubwa

Kocha wa timu ya taifa ya Canada, Jesse Marsch, amesema kikosi chake kiko tayari kukabiliana na presha ya kucheza michuano mikubwa mbele ya mashabiki wao wa nyumbani, huku akisisitiza kuwa wachezaji wake wamekuwa wakisubiri nafasi kama hiyo kwa muda mrefu.

Marsch Aipa Canada Moyo Kabla ya Mechi ya Ufunguzi wa Michuano MikubwaCanada itashuka dimbani Ijumaa katika mchezo wake wa kwanza wa mashindano haya makubwa Duniani wakiwa nyumbani dhidi ya Bosnia and Herzegovina kwenye Kundi B. Licha ya changamoto za majeraha zilizokikumba kikosi hicho katika maandalizi, Marsch amesema hana wasiwasi wowote kuhusu uwezo wa timu yake. “Kama hii ndiyo kazi yako, basi hapa ndipo unapopaswa kuwa. Nilikuja Canada kuwa kocha kwa sababu niliwaamini wachezaji hawa, lakini pia nilikuja kuwaongoza kwenye Kombe la Dunia la nyumbani. Nilihitaji jukumu hili,” alisema.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Habari kubwa zaidi kambini ni kuhusu nahodha Alphonso Davies, ambaye atakosa mchezo wa ufunguzi kutokana na jeraha la msuli wa nyuma wa paja alilopata akiwa na Bayern Munich mwezi uliopita. Hata hivyo, Marsch amesema vipimo vya MRI vilivyofanyika Jumatano vimetoa matumaini makubwa ya mchezaji huyo kurejea mapema. Hatakuwa tayari kwa mchezo wa kesho, lakini ameonyesha uwezo mkubwa wa kupona majeraha ya misuli. Tuna matumaini makubwa kwamba katika siku zijazo ataweza kurejea na kusaidia timu,” alisema.

Marsch Aipa Canada Moyo Kabla ya Mechi ya Ufunguzi wa Michuano MikubwaKocha huyo pia alituliza hofu kuhusu kiungo Ismael Kone, ambaye aliondoka mazoezini mapema Jumatano na kuzua taharuki miongoni mwa mashabiki. Marsch alieleza kuwa mchezaji huyo alikuwa akijisikia vibaya kidogo na kupelekwa nyumbani kwa tahadhari. “Watu walifanya suala hilo lionekane kama dharura kubwa. Ismael amefanya mazoezi leo, yuko sawa kabisa na yuko tayari kucheza,” alisema.

Marsch Aipa Canada Moyo Kabla ya Mechi ya Ufunguzi wa Michuano Mikubwa
Kuhusu beki Moise Bombito, ambaye amekuwa akirejea taratibu kutoka kwenye jeraha la mguu uliovunjika, Marsch alisema maendeleo yake ni mazuri na anaweza kuwa chaguo muhimu katika siku zijazo. “Bado hajafikia asilimia 100 ya utimamu wake, lakini tayari amerejea kwenye kasi yake ya juu. Sioni sababu ya kutokuwa tayari kuanza mchezo wiki moja ijayo,” aliongeza.

Marsch Aipa Canada Moyo Kabla ya Mechi ya Ufunguzi wa Michuano MikubwaMarsch pia amewakumbusha wachezaji wake umuhimu wa nidhamu, akibainisha kuwa kadi nyekundu zinaweza kuharibu safari ya timu yoyote kwenye mashindano makubwa. “Moja ya njia rahisi za kuharibu mashindano ni kupata kadi nyekundu. Tunapaswa kucheza kwa nguvu na kasi, lakini pia tunahitaji kutuliza hisia zetu na kuepuka makosa yasiyo ya lazima,” alisema. Kocha huyo alihitimisha kwa kuonyesha imani kubwa kwa kikosi chake, akisema: “Tuko tayari kucheza mechi kubwa, tuko tayari kuifanya nchi yetu ijivunie na tuko tayari kupambana kwa kila kitu tulicho nacho.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.