Martinez Amtetea Ronaldo Dhidi ya Wakosoaji Baada ya Sare na DR Congo

Kocha wa Ureno, Roberto Martinez, amesema kikosi chake hakina presha yoyote kuelekea mchezo wao wa pili wa michuano ya Dunia 2026 dhidi ya Uzbekistan, licha ya kukosolewa kufuatia sare ya mabao 1-1 dhidi ya DR Congo katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi K.

Martinez Amtetea Ronaldo Dhidi ya Wakosoaji Baada ya Sare na DR CongoUreno ilitawala umiliki wa mpira katika mchezo huo lakini ilishindwa kutumia nafasi ilizozitengeneza, ikipiga mashuti saba pekee huku moja tu likilenga lango. Martinez amesema timu yake ilianza vizuri mchezo huo lakini ilipoteza nidhamu ya kimfumo baada ya dakika 20 za mwanzo, jambo ambalo wamefanyia kazi kuelekea mechi inayofuata.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Sisi ni timu imara na yenye umakini mkubwa. Kundi letu lina umoja mkubwa zaidi sasa kuliko hapo awali. Kukosolewa baada ya matokeo yasiyoridhisha ni jambo la kawaida, lakini hilo halibadilishi namna tunavyojiandaa kwa mechi zetu,” alisema Martinez wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Martinez Amtetea Ronaldo Dhidi ya Wakosoaji Baada ya Sare na DR CongoKocha huyo pia alimkingia kifua nahodha Cristiano Ronaldo, ambaye alikosolewa kwa kiwango chake dhidi ya DR Congo na baadhi ya wadau kupendekeza aanzie benchi katika mchezo dhidi ya Uzbekistan. “Cristiano ni mmoja wa wachezaji bora katika kutengeneza nafasi kupitia harakati zake. Ameitumikia nchi yake kwa muda mrefu na bado anaendelea kujituma kwa ajili ya timu. Ni mfano wa kuigwa ndani ya kikosi chetu,” alieleza Martinez.

Martinez Amtetea Ronaldo Dhidi ya Wakosoaji Baada ya Sare na DR CongoMartinez amesisitiza kuwa Ureno inahitaji ushindi dhidi ya Uzbekistan ili kuendelea kushindana na Colombia, ambayo inaongoza Kundi K baada ya kuifunga Uzbekistan mabao 3-1. “Sote tulihuzunishwa na matokeo ya kwanza, lakini tunaamini kesho tutakuwa tayari kucheza kwa kiwango cha juu kwa dakika zote 90 na kupata matokeo tunayoyahitaji,” aliongeza kocha huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.