Martínez: Kumbukumbu ya Diogo Jota Inatupa Nguvu ya Kuifunga Croatia

Kocha wa Ureno, Roberto Martínez, amesema kikosi chake kitaingia kwenye mchezo wa hatua ya 32 Bora dhidi ya Croatia kikiwa na hamasa ya kipekee, huku kumbukumbu ya aliyekuwa mshambuliaji wao, Diogo Jota, ikiwa chanzo kikubwa cha motisha. Ureno ilimaliza nafasi ya pili katika Kundi K baada ya sare dhidi ya DR Congo na Colombia pamoja na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Uzbekistan.

Martínez: Kumbukumbu ya Diogo Jota Inatupa Nguvu ya Kuifunga CroatiaMartínez alisema maandalizi ya hatua ya mtoano ni mwanzo wa “michuano ya Dunia la pili,” akisisitiza kuwa mechi dhidi ya Croatia haitakuwa rahisi kutokana na uzoefu mkubwa wa wapinzani wao kwenye michuano hiyo. “Kesho tunaanza Kombe la Dunia la pili. Maandalizi ya hatua hii yalikuwa muhimu sana, na tunajua Croatia ni timu imara inayotufahamu vizuri kama tunavyoifahamu sisi,” alisema Martínez.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha huyo pia alitetea uamuzi wake wa kumchezesha dakika zote 90 nahodha Cristiano Ronaldo katika mechi iliyopita, akieleza kuwa kila mchezaji yupo tayari kuitumikia timu wakati wowote atakapohitajika. Aidha, aliwasifu Ronaldo na nahodha wa Croatia, Luka Modrić, akisema umri wao si kigezo bali mchango wao mkubwa ndani na nje ya uwanja.

Martínez: Kumbukumbu ya Diogo Jota Inatupa Nguvu ya Kuifunga Croatia“Umri ni namba tu. Kinachohesabika ni kile wanachokifanya uwanjani na mfano wanaouonyesha kwa wachezaji wenzao,” aliongeza Martínez.

Martínez: Kumbukumbu ya Diogo Jota Inatupa Nguvu ya Kuifunga CroatiaKiungo wa Ureno, Vitinha, alisema timu yote imejipanga kupambana kwa ajili ya familia zao, taifa la Ureno na kumuenzi Diogo Jota, huku akisisitiza kuwa ushindi dhidi ya Croatia utakuwa zawadi bora ya kumbukumbu yake. “Tutapambana kwa ajili ya familia zetu, kwa ajili ya Diogo Jota, na kwa ajili ya Ureno yote. Tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunashinda dhidi ya Croatia,” alisema Vitinha.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.