Beki wa Atletico Madrid, Matteo Ruggeri, amejikuta katikati ya mjadala mkubwa baada ya kuripotiwa kutuhumiwa kulipia ujumbe wa sauti wenye maudhui ya kibaguzi, kumkufuru Mungu na ya kingono kutoka kwa mwanamke kupitia mtandao wa Instagram. Tuhuma hizo zimeibua hisia kali miongoni mwa mashabiki huku zikisubiri uthibitisho rasmi.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, Ruggeri mwenye umri wa miaka 23 alidaiwa kulipa euro 150 ili apokee ujumbe maalumu wa sauti. Inadaiwa kuwa baadhi ya maombi yake yalihusisha kauli za kibaguzi, matusi dhidi ya Mungu pamoja na maudhui mengine yasiyofaa. Hata hivyo, hadi sasa mchezaji huyo hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akaunti ya Atletico Universe kwenye mtandao wa X ilidai kuwa Ruggeri aliomba ujumbe uliokuwa na kauli za kibaguzi na kumkufuru Mungu. Pia ilinukuliwa ikisema, “Ondoeni mchezaji huyu ndani ya klabu,” kauli iliyoonyesha hasira za baadhi ya mashabiki waliojitokeza kutoa maoni yao kufuatia kusambaa kwa madai hayo.
Picha za skrini na video zinazodaiwa kuhusiana na tukio hilo zimeendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, jambo lililozidisha mjadala kuhusu mustakabali wa beki huyo. Hata hivyo, uhalisia wa nyaraka hizo bado haujathibitishwa rasmi na mamlaka husika au klabu ya Atletico Madrid.
Kabla ya kuibuka kwa sakata hili, Ruggeri alikuwa akihusishwa na uwezekano wa kujiunga na AS Roma ili kuungana tena na kocha Gian Piero Gasperini. Hata hivyo, iwapo tuhuma hizi zitathibitishwa kuwa za kweli, zinaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa maisha yake ya soka na mipango yake ya uhamisho katika dirisha hili la usajili.


